Pages

BREAKING NEWS: RAIS JOHN POMBE MAGUFULI ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI

Magufuli: Tutakuwa na mawaziri 19, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na manaibu waziri. Lengo ni kuwa na baraza dogo kupunguza gharama. Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina elezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure.
 
WIZARA Ofisi ya Rais, Tamesemi utumishi na utawala bora, Simbachawene na Kairuki, Naibu waziri Jaffo Mazingira: Makamba Ajira, walemavu: Jenista Mhagama, Naibu nimemtua mbunge, Pos Abdallah ambae ni mhadhiri Dodoma Ulemavu: Mavunde Kilimo, mifugo na uvuvi: Mwigulu Lameck Nchemba, Nashe naibu Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano: Waziri bado sijamtafuta, naendelea kumfikiria, Naibu waziri Ngonyani. Fedha na mipango: Waziri bado, naibu Kijachi Nishati na madini: Waziri ni Muhongo, Naibu Katiba na sheria: Waziri Mwakyembe Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki: Augustino Mahiga nmemteua mbunge na waziri, Naibu Dr Suzan Ulinzi na kujenga taifa: Waaziri Dr. Hussein Mwinyi Ardhi na maendeleo ya makazi: Waziri ni Wiliam Lukuvi, Naibu Angelina Mabula Utalii: Waziri bado Viwanda na biashara: Waziri Charles Mwijage Sayansi na ufundi: Naibu ni Stella Manyanya Afya na Ustawi wa jamii: Ummy Mwalimu, Naibu ni Kingwangala
Habari: Nape Nnauye Wizara ya maji na umwagiliaji: Makame Mbarawa, Naibu ni Kamwene Swali: Tatizo ni nini hasa kwa wizara ambazo hujateua? Magufuli: Nilitegemea ungeniuliza kwanini sikuteua siko niliyoteuliwa, subira yavuta heri, hawa wameanza na wengine watafata Umesema kukutakuwa na semina elekezi, utafanya nini waweze kwenda na kasi ya hapa kazi? Niliyowachagua wote wana CCM na walinadi ya sera hapa kazi, spidi ni hiyo hiyo ndio maana hatutatumia semina elekezi ya bilioni mbili. Manyerere Jackton: Kwa kupunguza baraza la mawaziri, serikali itakuwa imepunguza kiasi gani? Magufuli: Wewe ndie utapiga hesabu, utanisaidia katika kupunguza baraza tutakuwa tumesevu kiasi gani na zile tulizosevu za gharama elekezi, kuchelewa kutangaza baraza na wale ambao sijawataja na bahati nzuri nyie waandishi mnaweza kupiga hesabu vizuri. Zipo nchi zina wizara 44, manaibu na mawaziri. Tutakapomaliza tutakuwa na baraza la watu 34. Wasihangaike kufanya sherehe kwa sababu ni kazi ngumu, wakawafanyie kazi watanzania bila kuwabagua, mawaziri hili la wizara 15 tumejiridhisha linaweza kufanya kazi tunayowatarajia kuifanya. Ngoja tukimaliza uteuzi wote. Uhai Production: Siku saba zimetimia, wafanyabiashara wamesharesha zile hela? Magufuli: Swali hilo jibu analo kamishna wa kodi TRA Swali: Katika baraza, kuna mawaziri wa baraza lililopita, ulizangatia nini wakati wa uteuzi? Jibu: Kafanye hesabu vizuri, waliorudi ni saba?

No comments:

Post a Comment

Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks